Idara

Idara ya Rasilimali za Maji

Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi na ina sehemu nne.

Majukumu yake ni kusimamia na kufuatilia wingi na ubora wa rasilimali za maji pamoja na usalama wa mabwawa. Vilevile, kukusanya takwimu za kihaidrolojia pamoja na za matumizi ya maji; kuandaa ramani za kihaidrolojia, kuandaa vibali vya matumizi ya maji; ukaguzi wa vyanzo vya maji na kuweka mipango ya utafiti wa vyanzo vya maji pamoja na usimamizi wa mazingira ya vyanzo vya maji na kutoa msaada wa kiufundi na elimu ya uhamasishaji juu ya ujenzi wa visima, uhandisi wa masuala ya maji, usimamizi wa maeneo ya matukio na matumizi sahihi ya vyanzo vya maji.

Kazi zake:-

-Kusimamia na kuandaa Sera ya Maji pamoja na utekelezaji wake;

-Kusimamia matumizi endelevu ya maji;

-Kusimamia maendeleo na usimamizi sahihi wa vyanzo vya maji kulingana na sera na mikakati;

-Kukusanya taarifa za kihaidrojeolojia na kihaidrometolojia na kuzisambaza kwenye taasisi za Serikali na Umma;

-Kuzijengea uwezo Sekretarieti za Maji;

-Kuratibu ushiriki wa Wizara katika mijadala ya maendeleo kitaifa na kimataifa, usimamizi pamoja na matumizi ya rasilimali za maji shirikishi;

-Kutoa miongozo kwa wadau kuhusu usanifu na ujenzi wa mabwawa na usimamizi wa hifadhi za maji.

Idara ina sehemu tatu na Bodi ya Maji iko chini ya Idara hii:-

Sehemu ya Usimamizi na Tathmini ya Rasilimali za Maji

-Kutoa miongozo na viwango vya upatikanaji wa takwimu za kihaijeolojia na kihaidrometolojia;

-Kusimamia Benki ya Takwimu za rasilimali za maji za hapa nchini;

-Kusimamia kazi za Ofisi za Mabonde na kutoa msaada wa kiufundi katika kusimamia, kuratibu na kuendeleza kazi za rasilimali za maji;

-Kutoa miongozo na viwango vya usanifu na ujenzi wa mabwawa;

-Kuwasiliana na Wakala ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) juu ya utabiri wa hali ya hewa pamoja na mifumo ya tahadhari na kuzitawanya taarifa kwa umma.

Sehemu ya Mipango, Utafiti na Maendeleo ya Rasilimali za Maji

-Kuratibu mipango shirikishi ya maendeleo na matumizi ya maji katika Sekta ya Maji;

-Kutafiti na kuendeleza vyanzo mbalimbali vya maji;

-Kuhifadhi na kusambaza taarifa mbalimbali za vyanzo vya maji;

-Kuratibu na kufanya tafiti zinazohusiana na ya maendeleo ya vyanzo vya maji.

Sehemu ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Shirikishi

-Kuratibu ushiriki wa Wizara katika mijadala ya kitaifa na kimataifa inayohusu uanzishwaji wa miradi ya maendeleo na kuendeleza matumizi ya maji shiriki;

-Kuratibu na kuandaa utekelezaji wa miradi na usimamizi wa rasilimali za maji shirikishi.

Sehemu ya Uhifadhi wa Vyanzo vya Maji

-Kutoa miongozo na msaada kwa ofisi za mabonde juu ya utekelezaji wa sheria na matumizi ya maji ikiwemo sheria juu ya uchimbaji visima na utafiti wa maji chini ya ardhi;

-Kusimamia daftari la haki za maji, jumuiya za watumiaji maji na makundi mengineyo;

-Kuratibu na kusimamia shughuli za uhifadhi wa rasilimali za maji.


Idara ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira

Lengo

Kusimamia huduma ya usambazaji maji na usafi wa mazingira.

Majukumu

(i) Kuandaa mipango ya muda mfupi, wa kati na muda mrefu kuhusu huduma za maji na usafi wa mazingira .

(ii) Kuandaa na kupitia Sera ya Maji pamoja na utekelezaji wa Sera na Mikakati hususani katika masuala ya huduma za maji na usafi wa mazingira kwa jamii;

(iii) Kuangalia utendaji wa watoa huduma za majisafi na usafi wa mazingira

(iv) Kuandaa kiwango na miongozo kuhusu menejimenti ya huduma za maji na usafi wa mazingira

(iv) Kuhamasisha maendeleo ya ukuaji wa huduma ya maji kwa jamii kulingana na Sera na Mkakati;

(v) Kusimamia utekelezaji wa programu za huduma ya maji kwa jamii;

Sehemu ya Msaada wa Huduma za Kiufundi

-Kutoa msaada wa kiufundi, kifedha na kuzijengea uwezo Halmashauri za Wilaya, ikiwamo uundaji wa vyombo vya watumia maji, kubuni, kuandaa, kujenga na kusimamia miradi ya maji;

-Kusimamia maandalizi na utekelezaji wa miradi ya maji ya kitaifa inayosimamiwa na Serikali moja kwa moja.

Sehemu ya Menejimenti na Msaada kwa Jamii

-Kusimamia uanzishwaji wa vyombo vya watumiaji maji kisheria ili kuwezesha usimamizi wa miradi ya maji vijijini;

-Kusaidia na kuwezesha ushiriki wa Sekta Binafsi na wadau wengine katika utoaji wa huduma ya maji na usafi wa mazingira.

Sehemu ya Mipango na Utekelezaji

-Kusaidia na kufuatilia maandalizi ya mipango na bajeti za Halmashauri za Wilaya katika masuala ya huduma za usambazaji maji safi na usafi wa mazingira;

-Kusaidia kutoa miongozo ya utekelezaji wa mikakati ya utoaji wa huduma ya maji vijijini kwa Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri za Wilaya na Wadau wengine.

Ubora wa Maji

Idara inaongozwa na Mkurugenzi na ina na vitengo vitatu.

Jukumu la idara ni kutoa huduma zinazohusu masuala ya usimamizi wa ubora wa maji. Idara ina mtandao wa maabara kumi na sita (16) katika mikoa ifuatayo; Arusha, Kagera, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kigoma, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Mara, Singida, Shinyanga, Ruvuma, Rukwa, na Tanga. Pia, ina kituo kimoja cha Utafiti wa Madini ya Floraidi kilichopo Ngurdoto, Arusha.

Kazi zake:-

-Kushiriki katika kuandaa sera ya maji, kupitia viwango vya ubora wa maji, kutoa miongozo na maoni katika utekelezaji wa mikakati ya usimamizi wa ubora wa maji.

-Kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu usimamizi wa ubora wa maji.

-Kutoa ushauri kuhusu tafiti mbalimbali zinazohusu ubora wa maji.

-Kutoa ushauri wa kiufundi kwenye mitambo ya kusafisha maji na uidhinishaji wa ubora wa madawa ya kusafisha maji.

Sehemu ya Uratibu wa Ubora wa Maji

-Kushiriki katika kutunga sera za ubora wa maji, viwango, sheria na miongozo kuhusiana na ubora wa maji.

-Kuratibu na kutoa miongozo kuhusu ufuatiliaji wa ubora wa maji; ikiwa ni pamoja na majitaka na utuaji anga – (atmospheric depositioning).

-Kutayarisha, kuboresha, kutunza takwimu za ubora wa maji na kusambaza taarifa zake.

-Kutathmini na kutoa ripoti za viwango vya ubora wa maji

-Kushauri kuhusu mipango na utekelezaji ya usimamizi wa ubora wa maji.

Sehemu ya Uhakiki na Viwango vya Ubora wa Maji

-Kushiriki katika kutunga Sera za ubora wa maji, Sheria na Miongozo kuhusiana na uhakiki na viwango vya ubora wa maji.

-Kutayarisha na kupitia miongozo na viwango vya utendeshaji kazi nje na ndani ya maabara za maji. Pia, kusimamia utekelezaji wa miongozo hiyo.

-Kusimamia na kuthibiti mipango kuhusu tathimini ya ubora wa maji.

-Kusimamia mchakato wa kupata ithibati kwa maabara za maji

-Kutoa ushauri kuhusu mapitio na uboreshaji wa viwango vya ubora wa maji na majitaka.

-Kutoa huduma kwa jamii na Sekta Binafsi kuhusiana na tathmini ya ubora wa maji na majitaka pamoja na ubora wa dawa za kusafisha maji.

-Kufanya majaribio kwa dawa zinazotumika kusafisha maji na kuidhinisha ubora wake.

-Kutoa ushauri wa kiufundi kwa viwanda kuhusu njia sahihi za kusafisha majitaka yanayotoka viwandani ili kuzuia uchafuzi wa vyanzo vya maji.

-Kuratibu masuala ya ushahidi wa kisheria kuhusiana na uchafuzi wa vyanzo vya maji

Sehemu ya Ushauri wa Kiufundi na Tafiti za Ubora wa Maji

-Kufanya tafiti na kutoa maoni katika kutayarisha Sera za ubora wa maji, Viwango, Sheria na Miongozo.

-Kutoa miongozo kuhusu usimamizi wa shughuli za tafiti zinazofanyika na kuhakikisha matokeo yake yanasambazwa.

-Kutoa miongozo kuhusu uondoaji wa masalia ya kemikali na madawa yaliyoisha muda wake wa matumizi.

-Kuhakikisha utekelezaji wa mipango ya usalama kazini ikiwa nje na ndani ya maabara za maji.

-Kutoa ushauri kuhusu mchakato wa kusafisha maji, upimaji wa madawa ya kusafisha na kuthibitisha ubora wake.

-Kutoa ushauri wa kitaalamu kwenye mitambo ya kusafisha maji kuhusiana na kiasi cha madawa kinachohitajika kusafisha maji.

Idara ya Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu

Idara inaongozwa na Mkurugenzi.

Kazi zake ni:-

-Kutoa mikakati ya kimenejimenti katika utawala na maendeleo ya rasilimali watu kama vile kuajiri, mafunzo, kuhamasisha kutoa huduma kwa watumishi na usimamizi wa utendaji;

-Kuhakiki usimamizi wa rasilimali watu katika Wizara;

-Kuunganisha kati ya Wizara na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika utendaji wa Menejimenti ya Utumishi wa Umma;

-Kutoa huduma ya maelezo na kutunza kumbukumbu za taarifa za rasilimali watu;

Sehemu ya Utawala

-Kutafsiri Kanuni za huduma za umma, Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma (Standing Order) na sheria zingine za kazi;

Kusimamia uhusiano mzuri wa wafanyakazi na ustawi pamoja na afya, usalama, michezo na utamaduni;

-Kutoa usajili, kuweka kumbukumbu za ofisi na huduma za wahudumu;
-Kusimamia masuala ya kanuni;

-Kutoa huduma za ulinzi, usafiri na mambo mengine ya kiutawala kwa ujumla;

-Kutekeleza mambo mbalimbali ikiwemo Anuai za Jamii, Wasiojiweza, Wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI;

-Kufuatilia utekelezaji wa ushiriki wa Sekta Binafsi katika Wizara;

-Kusimamia jukumu la utekelezaji wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa Wizara.

Sehemu ya Menejimenti ya Rasilimali Watu

-Kusimamia zoezi zima la ajira ikiwemo kukusanya, kuchagua, kuchukua, kuthibitisha kazini pamoja na uhamisho;

-Kusimamia maendeleo na mafunzo ya rasilimali watu;

-Kuratibu mafunzo ya awali na programu za utangulizi kwa waajiriwa wapya;

-Kuweka mipango ya rasilimali watu ili kujua mahitaji na idadi ya wataalamu walio chini ya Wizara;

-Kusimamia mishahara na kuandaa idadi ya watu wote walioajiriwa;

-Kusimamia utekelezaji wa malengo na mfumo wa wazi wa kupima utekelezaji wa watumishi wa Wizara.

Sera na Mipango

Idara inaongozwa na Mkurugenzi na ina sehemu tatu.

Majukumu ya Idara hii ni kuandaa Sera, kusimamia utekelezaji wake na kupima matokeo ya utekelezaji wa Sera.

Kazi zake ni: -

Kusimamia maandalizi ya Bajeti ya Wizara;

-Kusimamia na kupima utekelezaji wa shughuli za Sekta ya Maji ndani na nje ya Wizara ili kuona kama vigezo vya utekelezaji vilivyowekwa vinafuatwa;

-Kutoa miongozo ya kimaamuzi ya mipango ya baadaye ya Wizara;

-Kuhamasisha na kuwezesha sekta binafsi ili ziweze kuwekeza katika Sekta ya Maji;

-Kukusanya taarifa za Sekta ya Maji kwa ajili ya maamuzi ya Wizara;

-Kuhusika na maandalizi ya hotuba ya Wizara na taarifa ya mwaka ya hali ya uchumi;

-Kutoa utaalamu wa mkakati wa pamoja katika kupanga na kubajeti;

-Kuhakikisha mipango na bajeti za Sekta ya Maji zinawekwa katika mipango na bajeti ya taifa.

Sehemu ya Sera

-Kuratibu maandalizi na mapitio ya Sera za Wizara na kuziwianisha na Sera nyingine za Kitaifa;

-Kuratibu utoaji wa maoni na ushauri kuhusu Sera na Nyaraka za Baraza la Mawaziri zilizoandaliwa na Wizara nyingine.

-Kuandaa (Memorandum of Understanding) za miradi na programu kwa ajili ya ushirikiano na utafutaji wa fedha kimataifa;

-Kuandaa taarifa za utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na maoni ya Kamati za Bunge;

-Kuratibu maandalizi ya hotuba ya mwaka ya mpango wa bajeti wa Wizara.

Sehemu ya Mipango

-Kuratibu uandaaji wa mpango wa mwaka na bajeti ya Wizara kwa utekelezaji na mpango mkakati wa muda wa kati;

-Kuunganisha taarifa za miradi ya maendeleo, programu na mpango wa utekelezaji;

-Kuandaa mikakati ya utafutaji fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo;

-Kuwasiliana na Wizara ya Fedha na Mipango na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu mipango na bajeti ya Wizara na taratibu za upangaji wake;

-Kutoa miongozo ya kitaalam na kujenga uwezo kwa Wizara kuhusu uandaaji wa mpango mkakati na bajeti; na

-Kushiriki katika uchambuzi na uhamasishaji wa kazi zinazoweza kufanywa na Sekta Binafsi.

Sehemu ya Usimamizi na Ufuatiliaji

-Kufuatilia utekelezaji wa mpango wa mwaka na mpango mkakati wa muda wa kati wa Wizara;

-Kuandaa taarifa za utekelezaji (za wiki, mwezi, robo mwaka, nusu mwaka na za mwaka mzima za Wizara);

-Kukusanya, kutafiti na kuchambua takwimu muhimu zinazohitajika katika uandaaji na utekelezaji wa Sera, mipango na bajeti.

-Kushiriki katika maandalizi ya mipango, programu na kazi za Wizara ikiwemo utengenezaji wa malengo na viashiria vyake.

-Kutoa msaada wa kiufundi ndani ya Wizara, hii ni pamoja na usimamizi na ufuatiliaji katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara;

-Kufanya ufuatiliaji wa huduma inayotolewa na Wizara kwa wadau;

-Kufanya tafiti na tathmini ya mipango, miradi na program za Wizara; na

-Kufuatilia utendaji wa wakala za Wizara.

-Kuratibu mapitio ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara.

Sera na Mipango

Idara ya Sera na Mipango inaongozwa na Mkurugenzi na ina sehemu kuu tatu za Sera; Mipango na Bajeti; pamoja na Sehemu ya Tathmini na Ufuatiliaji. Majukumu ya Idara ni kama ifuatavyo:-

(i)Kuratibu uandaaji na kufanya mapitio ya Sera, Programu na Mkakati wa Sekta ya Maji;

(ii)Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji wa maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi;

(iii)Kuratibu uandaaji wa nyaraka za Baraza la Mawaziri za Sekta ya Maji na kutoa maoni kwa nyaraka za Sekta nyingine;

(iv)Kuratibu uandaaji wa Bajeti ya Wizara;

(v)Kuratibu na kupima utekelezaji wa shughuli za Sekta ndani na nje ya Wizara ili kukidhi vigezo vya utekelezaji vilivyowekwa;

(vi)Kutoa miongozo ya kimaamuzi ya mipango ya baadaye ya Wizara;

(vii)Kuhamasisha na kuwezesha sekta binafsi ili ziweze kuwekeza katika Sekta ya Maji;

(viii)Kukusanya taarifa za Sekta ya Maji kwa ajili ya maamuzi ya Wizara;

(ix)Kuratibu maandalizi ya Hotuba ya Wizara na taarifa ya mwaka ya hali ya uchumi;

(x)Kutoa utaalamu wa mkakati wa pamoja katika kupanga na kubajeti; na

(xi)Kuhakikisha mipango na bajeti ya Sekta ya Maji inawekwa katika mipango na bajeti ya Taifa.