Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira Vijijini (RUWASA)

Utangulizi

RUWASA ni ufupisho wa Rural Water Supply and Sanitation Agency. Ni Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira Vijijini iliyoanzishwa kwa Sheria Na. 5 ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira ya Mwaka 2019. RUWASA imeanza kazi mwezi Julai, 2019.

Majukumu ya RUWASA ni pamoja na;

  • Kusanifu na kusimamia ujenzi wa miradi ya maji vijijini
  • Kufanya utafiti kuhusu maji chini ya ardhi
  • Kuchimba visima na kujenga mabwawa
  • Kusajili na kuviwezesha vyombo vya watumiaji maji vijijini
  • Kuhamasisha sekta binafsi kushiriki katika maendeleo ya sekta ya maji vijijini
  • Kumshauri Waziri wa Maji kuhusu uendeshaji wa sekta ya maji vijijini