Habari
Wakurugenzi wa mamlaka ndogo za maji wapewa shule
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amefungua kikaokazi cha mafunzo kwa Wakurugenzi watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira za wilaya na miji midogo,.
Mafunzo hayo yanafanyika katika ukumbi wa wizara Mtumba
Katika hotuba yake Mhandisi Waziri ameeleza kufurahishwa na mafunzo hayo yanayolenga kuwajengea uwezo katika usimamizi bora wa mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira yatakayo wasaidia katika kutatua changamoto zakiutendaji katika maeneo yao ya kazi
Mhandisi Waziri amesisitiza masuala yatakayo wasaidia watendaji wa mamlaka hizo kuweza kufikia malengo yao ni pamoja na upenda na ushirikiano kwa kuzingatia maadili ya kazi na kuimarisha ushirikiano na mamlaka nyingine za serikali
Ili kutimiza azma ya kuwapatia wananchi huduma bora ya majisafi na salama kwa asilimia 95 mijini na 85 vijijini ifikapo 2025
Kitengo cha Mawasiliano