Habari
Uzinduzi wa Kampeni ya Kupanda Miti Rafiki kwenye Vyanzo vya Maji

Wizara ya Maji imeandaa Mkutano Mkuu wa nane (8) wa Bodi za Maji za Mabonde unaotarajiwa kufanyika tarehe 16 Novemba, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Eden Highlands, Jijini Mbeya. Kauli Mbiu ya Mkutano itakuwa ni “Utunzaji Endelevu wa Vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Jamii na Ukuaji wa Uchumi”.
Ufunguzi wa Mkutano huu utafanyika sanjari na uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti rafiki wa maji kwenye vyanzo vya maji hapa nchini. Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wizara ya Maji inatekeleza majukumu ya usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji kupitia Bodi za Maji za Mabonde. Bodi hizo zipo tisa (9) ambazo ni; Rufiji, Wami/ Ruvu, Pangani, Ruvuma na Pwani ya Kusini, Kati, Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika, Ziwa Rukwa na Ziwa Nyasa.
Wadau wote wanakaribishwa wakiwamo viongozi wote, wananchi pamoja na Wataalam wa Wizara ya Maji,Washirika wa Maendeleo, Bodi ya Maji ya Taifa, Bodi za Maji za Mabonde, Mamlaka za Majisafi na Usafiwa Mazingira nchini; Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara na Taasisi za Serikali, Asasi zisizo zaKiserikali, (AZAKI) Mashirika ya Dini, Elimu ya Juu na Utafiti, Sekta Binafsi, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), pamoja na wadau mbalimbali wa Sekta ya Maji kushiriki katikazoezi la kupanda miti kwenye vyanzo vya maji na kushiriki hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Kupanda miti rafiki wa maji kwenye vyanzo vya maji
Kitengo cha Mawasiliano