Habari

Imewekwa: Apr, 06 2022

​Taarifa kwa Umma

News Images

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amefanya mabadiliko ya uongozi katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Singida (SUWASA).

Kufuatia mabadiliko hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Singida (SUWASA) Mhandisi Patrick Nzamba amepangiwa kituo kipya cha kazi ambacho ni Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama-Sinyanga (KASHWASA). Mhandisi Nzamba anachukua nafasi ya Mhandisi Joshua Mgeyekwa ambaye amestaafu Utumishi wa Umma kwa mujibu wa taratibu za Utumishi.

Pili, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Dodoma (DUWASA), Mkurugenzi Sebastian Warioba amepangiwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Singida (SUWASA). Waziri Aweso (Mb) alimteua Bw. Warioba kuwa mkurugenzi mapema mwezi Januari 2022.

Florence Temba

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano