Habari
Dkt. Mpango aipongeza Wizara ya Maji kwa usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maji nchini

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango ameweka Jiwe la msingi la ujenzi wamradi wa maji wa Ibihwa, Wilayani Bahi, mkoa wa Dodoma.
Mhe. Dkt. Mpango ameipongeza Wizara ya Maji kwa usimamizi mzuri na utejelezaji wa miradi ya maji nchini.
Pamoja na pongezi hizo, amesisitiza kuongeza kasi ya uchimbaji wa visima ili wananchi wapate huduma ya majisafi na salama, na ahadi ya kukamilisha mradi wa maji wa Ibihwa ikamilike ifikapo tarehe 30 Septemba, 2024.
Akitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa mradi huo, Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amewahakikishia wananchi wa Kijiji cha Ibihwa kuwa, Wizara itakamilisha mradi huo kabla ya tarehe 30 Septemba, 2024 na huduma ya maji itafika katika mji wa Bahi.
Mradi wa Maji wa Ibihwa unatekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 709 na unasimamiwa na Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), utekelezaji wake ukiwa umefika asilimia 75 na umeanza kutoa huduma kwa wananchi, na utanufaisha wananchizaidi ya elfu nane wa Kijiji cha Ibihwa
Mradi wa Maji wa Ibihwa unatekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 709 na unasimamiwa na Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), utekelezaji wake ukiwa umefika asilimia 75 na umeanza kutoa huduma kwa wananchi, na utanufaisha wananchizaidi ya elfu nane wa Kijiji cha Ibihwa.
Kitengo cha Mawasiliano