Habari
Maji Wami Ruvu kunufaisha Mkata
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amesema Serikali imepanga kutumia Shilingi milioni 500 kwa ajili ya kuboresha tenki la maji lililopo kata ya Mkata liweze kuwahudumia wananchi wa kijiji cha Manga kilichopo kata ya Mkata, Wilayani Handeni mkoani Tanga kwa kuhifadhi maji kutoka Bonde la Wami/Ruvu.
Waziri Aweso amebainisha hayo Ijumaa ya leo Novemba 15, 2024 wakati wa siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano Mkoani Tanga ambapo amesema kuwa tenki hilo lenye uwezo wa kuhifadhi zaidi ya lita laki tano za maji linatakiwa liwe suluhu kwa wananchi wa Manga na maeneo yote ya Mkata.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Burian amemshukuru Waziri Aweso kwa juhudi zake za kupambania sekta ya maji akisifu kujitoa kwake na ubunifu wake.
Ameongezq kwa kusema asilimia ya upatikanaji wa maji mijini na vijijini imeendelea kuongezeka siku baada ya siku kutokana na juhudi za Serikali ya awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan na uongozi madhubuti wa Waziri Aweso.