Habari

Imewekwa: Oct, 01 2024

​Benki ya Dunia yaikubali miradi ya maji

News Images

Wataalamu wa Wizara ya Majina wawakilishi wa Benki ya Dunia wamekagua mradi wa maji wa Sange na Zahanati ya Masaika wilayaniPangani na kuridhishwa na utekelezaji wake.

Kazi hiyo inafanyikamkoaniTanga ikiwa niufuatiliaji wa miradi ya maji na usafi wa mazingira iliyo tekelezwa kupitia fedha za progamu ya lipa kwa matokeo (PforR)katika Sekta ya Maji.

Mradi wa maji Sange una thamani ya shillingi Milioni 540 na umeanza kuhudumia wananchi ambapo utekelezaji wake ni asilimia 90 .

Ujenzi wa mradi huoumehusisha tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 50000,ujenzi wa nyumba ya mtambo wa kusukuma maji na ujenzi wa vituo vya umma vyakuchotea maji 13 na ulazaji wa mabomba zaidi ya Mita 9,900.

Kwausafi wa mazingira katika Zahanati ya Masaika kazi imehusishaujenzi wa kichomea taka,eneo la kitakasa mikono,ujenzi wa vyoo vya watumishi na matundu ya vyoo kwa huduma ya wagonjwa ,ujenzi wa mnara na ununuzi wa tanki la kuhifadhia maji.

Wilaya ya Panganikwa sasa hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama imefikaasilimia 92 na wananchi wameshukuru serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt SamiaSuluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kufanikisha huduma ya maji kwa watu wote.

Kitengo cha Mawasiliano