Habari

Imewekwa: Jun, 17 2021

Aweso afanya kikao na Benki ya EXIM ya India kuhusu mradi wa maji wa miji 28

News Images

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amefanya kikao na Uongozi wa Benki ya Exim ya India kwa njia ya kieletroniki kuhusu mradi wa maji wa miji 28.

Kikao hicho kimefanyika tarehe 16 Juni, 2021.

Mhe. Aweso katika kikao hicho amesisitiza uharakishwaji wa kibali ambacho Benki ya Exim inatakiwa kukitoa ili kazi za ujenzi wa mradi huo zianze.

Kwa upande wa viongozi wa Benki ya Exim ya India wamekiri kuchelewa kutoa kibali kwa sababu ya mlipuko wa maradhi ya UVICO 19 katika nchi yao hivyo kulazimisha kufanya kazi wakiwa nyumbani.

Kikao hicho kilimalizika kwa viongozi wa Benki ya Exim ya India kukubali kuharakisha kutoa kibali ili kazi za ujenzi ziweze kuanza mara moja.

Mradi huo wa Miji 28 unathamani Dola za Marekani milioni 500 ikiwa ni moja kati ya mradi mkubwa na wa kihistoria utakaoleta mapinduzi makubwa katika sekta ya Maji hapa Tanzania.

[5:26 PM, 6/17/2021] Hab. Florense. Wizara Ya Maji: