Maji Week 2026

Siku ya Maji 2026

Wizara ya Maji imekuwa ikiratibu Wiki ya maji kitaifa kila mwaka hapa nchini kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya maji. Maadhimisho haya yanatokana na Azimio Na. 47/193 la Umoja wa Mataifa (UN) kuwa kila ifikapo Machi, 22 ya kila mwaka nchi wanachama ziadhimishe Siku ya Maji Duniani kwa pamoja.

Hii ni Katika kutambua umuhimu na thamani ya maji katika maisha ya binadamu na uchumi wa Dunia kwa ujumla

Lengo kuu la maadhimisho ya Wiki ya Maji nchini ni kuungana na Mataifa mengine katika kutathimni utekelezaji, mafanikio, changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi ya maji na kuainisha mikakati ya kuboresha na kuimarisha utoaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira na kusimamia utunzaji wa rasilimali ya maji nchini.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya siku ya maji Duniani kwa mwaka 2026 ni: "Water and Gender yaani kwa Kiswahili ni Maji na Jinsia”. Kauli mbiu hii inalenga uhusiano kati ya rasilimali za maji na usawa wa kijinsia.

WASHIRIKI

Washiriki zaidi ya 1,000 wanatarajiwa kuwepo kwenye maadhimisho ya Wiki ya Maji kwa mwaka 2026 ikiwemo wawakilishi wa Wizara za Kisekta, Mashirika ya Umma, Wadau wa Maendeleo, Asasi za Kiraia, Taasisi za Serikali na zisizokuwa za Serikali, Sekta binafsi, Viwanda, Mashirika ya Dini, Taasisi za Fedha, Vyuo vya elimu ya juu, vyuo vya ufundi na jamii katika maeneo ya miradi.

Maadhimisho ya wiki ya Maji kwa mwaka 2026 yatafanyika katika mkoa wa Morogoro kwani ni kitovu cha kuzalisha maji na vyanzo vingi ikiwemo mito inayolisha mto Ruvu ikiwa ni tegemeo na manufaa ya mikoa miwili ya Pwani na Dar es Salaam na ni rahisi kufikika.


Hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi Bwawa la Kidunda

Mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe Wazinduliwa

Maji Kuwafikia Wananchi kwa Asilimia 100

Mkutano wa Mapitio ya Programu ya Sekta ya Maji

Siku ya EWURA 2025: Tuzo kwa Mamlaka za Maji

Muhtasari wa Utendaji wa Mamlaka za Maji 2023/24

Water Utilities Performance Review 2023/24

Maadhimisho ya Wiki ya Maji Kitaifa 2024

International Maji Scientific Conference 2024 : Call for Abstracts and Workshop Proposals

Kuelekea Siku ya Maji Duniani 2023

Siku ya Maji Duniani Kitaifa

Taarifa kwa Umma

Uzinduzi wa Wiki ya Maji 2022

Wiki ya Maji: 2020

Taarifa kwa Umma: Kusitisha Shughuli Kueleka Siku ya Maji Duniani

Taarifa kwa vyombo vya Habari: Wiki ya Maji

Wiki ya Maji 2020: Mwisho wa kujisajili ni tarehe 20 Februari, 2020; Bofya kiunganishi kujisajili

Second call for Abstracts/Call for Sessions: 2020 Maji (Water) Week Annual Scientific Conference

Maji Week Exhibition: Dar es salaam, click this link for details