Habari
Bwawa la Kidunda Kuzalisha Lita Bilioni 20 kwa Siku, Kuwa Suluhu ya Changamoto ya Maji Jijini Dar
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb), amesema Bwawa la Maji la Kidunda linatarajiwa kuwa na uwezo wa kuzalisha hadi lita bilioni 20 za maji kwa siku kwa ajili ya huduma ya majisafi na salama.... Soma zaidi
Imewekwa: Dec 17, 2025
Serikali Yataka Mradi wa Maji Mafinga Ukamilike kwa Kasi na Ubora
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Kundo Andrea Mathew (Mb), amemtaka mkandarasi wa Mradi wa Maji wa Miji 28 Mafinga, Kampuni ya Jandu Plumbers Ltd, kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha wananchi wa Mafinga wanapata huduma ya maji safi na salama kwa wakati uliopangwa.... Soma zaidi
Imewekwa: Dec 15, 2025
Kundo Aagiza Taasisi Zote Za Sekta Ya Maji Njombe Kuboresha Huduma
Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, amezitaka taasisi zote za sekta ya maji mkoani Njombe kufanya tathmini ya kina na kuwasilisha takwimu sahihi kuhusu hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo wanayoyahudumia.... Soma zaidi
Imewekwa: Dec 15, 2025
Tanzania Yaunga Mkono Uendelevu wa Bonde la Mto Nile
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesisitiza msimamo wake thabiti wa kuendelea kuiunga mkono Jumuiya ya Bonde la Mto Nile (Nile Basin Initiative – NBI), ikibainisha kuwa rasilimali za maji katika bonde hilo ni msingi muhimu wa uchumi, usalama wa chakula na ustawi wa jamii katika nchi zote wanachama.... Soma zaidi
Imewekwa: Dec 08, 2025
Mto Ruvu Ubaki Kwa Matumizi ya Binadamu Tu – RC Kunenge
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge, ametoa wito kwa wakulima wanaotumia maji ya Mto Ruvu kwa shughuli za kilimo kusitisha matumizi hayo kwa muda, hadi pale mvua zitakapoanza kunyesha kwa wingi.... Soma zaidi
Imewekwa: Dec 08, 2025
Visima vya Akiba Vyaunganishwa Kwenye Mfumo wa Maji Ili Kupunguza Changamoto Dar
Waziri wa Maji, Mhe. Juma Aweso (Mb), amewataka wakazi wa Dar es Salaam na Pwani kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki cha upungufu wa maji, akibainisha kuwa hali hiyo ni ya mpito na inashughulikiwa kwa kasi.... Soma zaidi
Imewekwa: Dec 08, 2025
