Wasifu

Mhe. Jumaa H. Aweso (Mb)

Waziri wa Maji

Mhe. Jumaa H. Aweso (Mb)

Wasifu

Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso (Mb) alizaliwa tarehe 22 Machi 1985, Pangani, Mkoani Tanga. Mheshimiwa Aweso alisoma katika Shule ya Msingi ya Mwambao, Pangani, Mkoani Tanga (1994-2000) na Elimu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Bagamoyo (2001-2004). Mhe. Aweso alipata Elimu ya Juu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari ya Pugu (2005-2007).

Kati ya mwaka 2007 na 2009, Mheshimiwa Aweso alihudhuria Chuo cha Ualimu cha Morogoro na kutunukiwa Astashahada ya Ualimu. Mheshimiwa Aweso ana Shahada ya Sayansi katika Kemia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliyotunukiwa mwaka 2013. Mwaka 2018-2020 Mheshimiwa Aweso alihudhuria na kuhitimu Shahada ya Pili ya Utawala na Uongozi (Governance and Leadership (MAGL) ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Pangani lililopo Mkoani Tanga mwaka 2015. Mwezi Oktoba 2017, Mhe. Aweso aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, akichukua nafasi ya Mhe. Kamwelwe aliyeteuliwa kuwa Waziri.

Oktoba 2020, Mhe. Jumaa Hamidu Aweso alipita bila kupingwa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mbunge wa Pangani kwa Awamu ya Pili, 2020-2025. Mwezi Desemba 2020, aliteuliwa kuwa Waziri wa Maji.