Habari
Mradi wa Maji Dambia Haydom kuwafikia Dongobesh
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Kundo Mathew (Mb) amewahakikishia wananchi wa mkoa wa Manyara kuwa mradi wa Maji wa Dambia Haydom utakamilika na kuendelezwa hadi mji wa Dongobesh.
Amesema mradi huo pamoja na miradi mingine inayoendelea mkoani hapo ni Moja ya mikakati ya serikali kuhakikisha wananchi wa Mkoa wa Manyama wanafaidi matunda ya juhudi za Serikali za kumtua mama ndoo ya Maji kichwani.
Mhe. Kundo ameyasema hayo katika ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mwigulu Nchemba wilayani Mbulu.
Amesema miradi ya Maji ambayo ilichelewa kwa sababu mbalimbali tayari imepatiwa ufumbuzi na itatekekezwa na kukamilika ili kuyafikia malengo ya Serikali ya kufikisha huduma ya Majisafi na Salama kwa kila mwananchi katika umbali unaokubalika.

