News
Mradi wa maji Makonde kufuta adha ya maji Nanyamba
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesema serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa maji Makonde ambao unatarajiwa kuondoa kabisa changamoto ya huduma ya maji katika mji wa Nanyamba na maeneo mbalimbali mkoani hapo.
Mhe. Aweso ameyasema hayo katik ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi katika Kijiji cha Maranje, Halmashauri ya Mji Nanyamba.
Amesema mradi huo ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa katika miji 28 nchini Tanzania na unagharama ya shilingi bilioni 84.7 ambapo tayari bilioni 23.5 zimeshatolewa.
Amewahakikishiwa wananchi wa Mji wa Nanyamba na meneo mbalimbaIi ya mkoa wa Mtwara kuwa shilingi bilioni Nne itatolewa mwisho wa mwezi huu huku mwezi ujao ikitarajiwa kutolea tena bilioni 4 kwa lengo la kuharakisha utekelezaji.
Awali wakizungumza katika maeneo mbalimbali katika ziara hiyo, wabunge wa majimbo ya Newala, Tandahimba na Mtwara wameomba kuharakisha utekelezaji wa mradi huo huku wakionesha matumaini makubwa kutokana na uthubutu uliooneshwa na serikali katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maji mkoani hapo.
Mradi wa maji wa Makonde unatarajia kunufaisha halmashauri Nne za Newala Mji, Newala Wilaya, Tandahimba na Halmashuri ya Mji wa Nanyamba zenye jumla wakazi 640,000.

