Habari
Miradi ya Maji ya Mugeta na Nyang'aranga Yaundiwa Tume

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameunda timu ya kuchunguza miradi ya maji ya Mugeta na Nyang‘aranga iliyopo Bunda kutokana na miradi kutofanya kazi vizuri.
Akihutubia wananchi wa Bunda vijijini Naibu Waziri Aweso alilazimika kuunda timu hiyo itakayopitia miradi yote iliyoanishwa na kutoa taarifa ya changamoto na namna ya kuzitatua.
Timu hiyo ya ufatiliaji itaongozwa na Meneja wa RUWASA Mkoa wa Mara Mhandisi Muhibu Lubasa. Wajumbe wengine ni kama ifuatavyo:
Mhandisi Button Kajigili kutoka — MUWASA
Mhandisi Lucas Kivegalo kutoka — MUWASA
Mheshimiwa Myanga Gongola — Diwani
Bw. Oxygen Mang’ena — Katibu wa Kijiji Mugeta
Bw. Bernad Chigela — katibu wa Kijiji Nyang’aranga
Bw. Chacha Sabule — Mwananchi
Bw. Donald Peter — Mwananchi
Bi. Wankyo Mages — Mwananchi
Kuundwa kwa timu hiyo kumekuja baada ya malalamiko ya pande mbili baina ya wananchi wakiongozwa na viongozi wao kwa upande mmoja na wataalamu wa maji.
Wananchi walisema kuwa miradi hiyo imejengwa chini ya kiwango ndiyo maana haitoi maji ipasavyo, kwa upande mwengine, wataalamu wa maji walionesha hujuma zinazofanywa na watu wenye nia mbaya ya miradi ya maji.
Baadhi ya hujuma hizo zilizoeneshwa na wataalamu wa maji ni pamoja na kukatwa kwa uzio kwenye vyanzo vya maji, kutobolewa kwa bomba kwa vitu vyenye ncha kali, kukatwa kwa mabomba, visima kujazwa mawe na miti ili visitumike na kukata waya wa umeme kwenye pampu ya kusukumia majiKitengo cha Mawasiliano