Wasifu

Obadia Kibona

Kaimu Mkuu Kitengo cha Usimamizi wa Mazingira

Obadia Kibona

Bw. Obadia Kibona ni Mtaalamu wa Mazingira aliyesajiliwa na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) la Tanzania mwenye Usajili No. NEMC/EIA 0176 na cheti cha kuandaa taarifa za Tathimini za Athari kwa Mazingira (TAM), cheti Na. NEMC/PC/EIA/2022/0025. Amekuwa akifanya kazi na Sekta ya Maji tangu mwaka 2005. Ana uzoefu wa kufanya kazi katika nyanja za Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Kijamii, uandaaj wa mpango wa utekelezaji wa makazi mapya katika miradi, Ikolojia ya Majini na masuala ya kijamii na kiuchumi ya Maji, Uchafuzi na Udhibiti wa Mazingira, Usimamizi wa Maji ya Chini ya Ardhi na taka ngumu na mabadiliko tabianchi.

Ana ujuzi na uzoefu wa ngazi wa viwango vya Kimataifa katika kusimamia masula ya mazingira na iamii kupitia, uzoefu huu ameupataka kutoka na kusimamia masuala ya Mazingira na jamii katika miradi ya maji inayofadhiliwa na Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), mashirika yote haya licha ya kuwa na miongozo yao, bado yanazingatia viwango vya kimataifa (IFC) na Benki ya Dunia.

Aidha, Bw. Obadia ana cheti cha Uongozi kwa Vijana Wataalamu katika Sekta ya Maji alichokipata kutoka Chuo cha Uongozi na Menejimenti cha Saxony ya Chini Ujerumani (DMAN) mwaka 2020. Ana cheti cha Utafutaji na Uendelezaji wa maji ya chini ya ardhi alichopakipata Seoul-Korea ya Kusini (2008). Bw. Obadia ni mhitimu wa Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Mazingira katika taaluma ya Mipango na Usimamizi wa Mazingira (2008-2010) kutoka Taasisi ya UNESCO-IHE ya Elimu ya Maji iliyopo katika mji wa Delft nchini Uholanzi; na ana Shahada ya kwanza ya Sanaa katika Masomo ya Jiografia na Mazingira kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania (2002-2005).