Wasifu

Prosper Buchafwe

Mkurugenzi Msaidizi Sera na Mipango

Prosper Buchafwe

Prosper Mkama Buchafwe ni Mchumi anayefanya kazi ya uchambuzi, uandaaji na uratibu wa mipango, bajeti na maandiko ya miradi katika Idara ya Sera na Mipango Wizara ya Maji. Alizaliwa mkoani Mara na katika safari yake ya masomo alisoma shule ya msingi na sekondari wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Bwana Buchafwe ana Shahada ya Uzamili (Masters in Security and Strategic Studies) kutoka Chuo Cha Ulinzi Cha Taifa Dar es Salaam Tanzania, Shahada ya Uzamili (Masters of Public Policy in Economic Development) kutoka KDI Seoul South Korea, Shahada ya Uchumi Kilimo (Bsc. in Agricultural Economics and Agribusiness) kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine kilichoko mkoani Morogoro Tanzania.

Kabla ya kuhamia Wizara ya Maji mwezi Novemba 2019, alifanya kazi Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa katika nafasi ya Mchumi na baadaye kuteuliwa kuwa Kamishna Msaidizi Sehemu ya Sera Agosti, 2012.