Wasifu

Eng. Nadhifa Kemikimba

Mkurugenzi, Idara ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira

Eng. Nadhifa Kemikimba

Mhandisi Nadhifa Sadiki Kemikimba aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Ubora wa Maji tarehe 15 Novemba, 2010. Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Kemikimba alifanya kazi katika Idara ya Huduma za Ubora wa Maji kuanzia ngazi za kiufundi moaka uongozi wa idara inayosimamia masuala ya ubora wa maji wizarani.

Mhandisi Kemikimba alizaliwa tarehe 26 Septemba, 1966 mkoani Kagera na Elimu za Msingi na Sekondari amesomea mkoani humo hadi alipojiunga na Chuo cha Maji (Rwegarulira) kilichopo jijini Dar es Salaam mwaka 1986-1989 na kuchukua masomo ya Teknolojia ya Maabara ya Maji.

Mwaka 1994 alipata Stashahada ya Uhandisi wa Mazingira kutoka Chuo cha Ardhi (kwa sasa ni Chuo Kikuu cha Ardhi) na mwaka 2006 alipata Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Maji katika Usimamizi wa Ubora wa Maji kutoka chuo cha UNESCO-IHE Delft nchini Uholanzi. Tangu mwaka 1989 Mhandisi Kemikimba ni mwajiriwa wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.