Wasifu

Simon Nkanyemka

Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Sheria

Simon Nkanyemka

Wakili Simon S. Nkanyemka ni Mwanasheria anayefanya kazi ya kuishauri wizara na taasisi zake katika masuala yote ya kisheria yanayohusu utekelezaji wa majukumu ya wizara na kuwasiliana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika masuala ambayo kwa mujibu wa sheria au utekelezaji wake yanapaswa kupata maoni ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Ana Shahada ya Uzamili katika Sheria za Mashirika na Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (2013) na Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (2004). Wakili Simon amesajiliwa kuwa Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na mahakama za chini isipokuwa mahakama za Mwanzo tangu mwaka 2009. Alimaliza elimu ya sekondari ya juu katika Shule ya Sekondari Pugu iliyopo Mkoani Dar es Salaam (1995 – 1997) na alihitimu elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora iliyopo Mkoani Tabora (1991 - 1994). Aidha, alipata mafunzo mbalimbali katika masuala ya uandishi wa sheria, uendeshaji wa mashauri mahakamani, mikataba na mbinu za majadiliano hivyo kuwa na umahiri katika masuala hayo..

Aliteuliwa kushika nafasi ya Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria mwaka 2012.