Habari

Imewekwa: Oct, 04 2019

Simiyu yapata mradi wa maji

News Images

Ujumbe wa Bunge la Ujerumani ulioongozwa na Mheshimiwa Sylia Kotting-Uhl wamefanya ziara Mkoani Simiyu kwa ajili ya kutembelea maeneo yatakayojengwa mradi wa maji wakukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi (Simiyu Climate Resilience Water Supply Project) utakaonufaisha wananchi zaidi ya laki nane wanaoishi katika halmashauri zote za Mkoa wa Simiyu.

Naibu Waziri wa Maj,i Mheshimiwa Jumaa Aweso (Mb) amesema kuwa mradi wa maji wa Simiyu utajengwa kwa gharama ya zaidi ya bilioni mia nne ambazo zitachangiwa na Wadau wa Maendeleo, Serikali ya Ujerumani na Serikali ya Tanzania pamoja na nguvu kazi za wananchi wa Simiyu.

Utekelezaji wa mradi huu utakuwa kwa awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza itahusu wilaya za Busega, Bariadi na Itilima wakati awamu ya pili itahusu wilaya zote zitakazokuwa zimebaki.

Lengo kuu la mradi ni kuboresha afya na kuongeza uzalishaji mali ili kuinua hali ya maisha kwa wananchi walioathirika na mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo husika ya mradi.

Kazi zitakazofanyika katika mradi huu ni pamoja na; kupeleka huduma ya majisafi na ya uhakika pamoja na kupanua mfumo wa usambazaji maji katika vijiji na maeneo lengwa ya mradi.

Pia mradi utakarabati na kujenga mabwawa ya kilimo cha umwagiliaji endelevu (Smart Agriculture) pamoja nakuimarisha huduma ya usafi wa mazingira hususan ujenzi wa mabwawa ya majittaka(sludge digester) na vyookatika maeneo ya shule na vituo vya afya.

Kitengo cha Mawasiliano