Bohari Kuu ya Maji

Jukumu lake kuu ni kuhakikisha vifaa na vitendeakazi vinavyohitajika kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya majisafi na majitaka vinapatikana kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.

Vilevile inahusika na upatikanaji wa Mafuta ya Petroli na Diseli kwa ajili ya magari ya Serikali.

Kazi zingine ni pamoja na

  • Kuwezesha ununuzi wa vifaa vya miradi ya maji vyenye ubora;
  • Kusambaza vifaa mbalimbali kwa wateja kwa ajili ya utekelezaji wa programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji.