Habari

Imewekwa: Jul, 15 2019

Taarifa kwa Vyombo vya Habari - Uteuzi

News Images

Waziri wa Maji Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) amefanya uteuzi wa Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama pamoja na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora na Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba.

Waziri Prof. Mbarawa amefanya uteuzi huo baada ya kufanya ziara ya kikazi katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Kagera ambapo ameona changamoto mbalimbali kuhusu huduma ya maji.

Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;

  • Eng. Joel Rugemalila aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora
  • Bw. Allen Marwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama na
  • Eng. Clavery Toto aliyekuwa Meneja Ufundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba atakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba.

Prof. Mbarawa amesema zoezi la uteuzi wa Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Maji nchini hususan waliokaa kituo cha kazi kimoja kwa muda mrefu litakua endelevu ili kupata matokeo chanya katika sekta ya maji nchini.

Kitengo cha Mawasiliano

15 Julai, 2019