Wasifu

Eng. Lydia Joseph

Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji na Utoaji Huduma

Eng. Lydia Joseph

Mkurugenzi Msaidizi Lyidia Joseph ni Mhandisi Ujenzi aliyesajiliwa na Bodi ya Wahandisi nchini na amehitimu Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Rasilimali za Maji katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Amewahi kufanya kazi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida kabla ya kujiunga na Wizara ya Maji mnamo mwezi Agosti, 2018.

Nafasi yake katika Wizara ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Utoaji wa Huduma na Uendeshaji wa Vyombo vya Watumiaji Maji.

Ana uwezo mkubwa wa kuanzisha jambo na kulisimamia hadi lifanikiwe. Anapendelea kujifunza mambo mapya na kufanya kazi kwa bidii.