Wasifu

Ahadi Msangi

Mhasibu Mkuu

Ahadi Msangi

Ahadi E.Msangi alihamishiwa Wizara ya Maji na Umwagiliaji mwezi April, 2017 kushika nafasi ya Mhasibu Mkuu. Kabla ya kujiunga na Wizara ya Maji na Umwagiliaji alifanya kazi katika Wizara ya Elimu (kati ya Novemba 2016 –April 2017); Wizara ya Nishati na Madini (Kati ya Mei 2012 – Novemba 2016); Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Kati ya Mei 2010 – April 2012); Wizara ya Fedha na Mipango (Kati ya Septemba 2006 – April 2010) katika nafasi ya Mhasibu Mkuu.

Kabla ya kuteuliwa katika nafasi ya Mhasibu Mkuu katika Wizara ya Fedha na Mipango alifanya kazi katika sehemu mbali mbali kwenye wizara hiyo kati ya mwaka 1997 hadi 2006. Kabla ya kujiunga na Wizara ya Fedha na Mipango alifanya kazi Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa kama Mhasibu.

Ameshiriki katika utekelezaji wa Programu ya Maboresho ya Sekta ya Fedha (Public Financial Management Reform Programme) awamu ya kwanza hadi ya tatu (1998-2012) ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa ofisi ya malipo ya pamoja (Central Payment Office) Zanzibar, malipo ya Serikali kwa njia ya Kielectroniki na sehemu ya “Cash Management” Wizara ya Fedha na Mipango.

Bw. Msangi ana Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Biashara (MBA) akibobea katika Fedha kutoka katika Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza aliyoipata mwaka 2009; Shahada ya Juu ya Uhasibu CPA (T) mwaka 1996. Vile vile ana Shahada ya Sheria (LLB Hons) kutoka katika chuo kikuu Huria Tanzania (OUT) aliyoipata mwaka 2014 na Stashahada ya Uhasibu kutoka chuo cha Uhasibu (Tanzania Institute of Accountancy) kilichojulikana awali kama “Dar-es-Salaam School Accountancy” mwaka 1990.

Alizaliwa tarehe 01/12/1964 Mwanga, mkoani Kilimanjaro na alisoma Shule ya Msingi Pasua, Moshi (1974 – 1980); Shule ya Sekondari Mawenzi, Moshi (1981 - 1984) na baada ya hapo alijiunga na kidato cha tano na sita katika shule ya Shycom Shinyanga (1985 -1987) na baada ya hapo alijiunga na JKT kwa mujibu wa sheria katika kambi za Msange Tabora na Itende Mbeya (1987-1988).