Wasifu

Naomi Lupimo

Mkurugenzi Msaidizi DWR Utunzaji wa Rasimali za Maji

Naomi Lupimo

Bi. Naomy Nyangeta Lupimo ni Mhaidrojiolojia anayefanya kazi katika Wizara ya Maji na Umwagiliaji kama Mkurugenzi Msaidizi. Aliajiriwa kwa mara ya kwanza katika Wizara ya Maji na Nishati kama Mhaidrojiolojia Msaidizi mwaka 1984 hadi 1986. Mwaka 1987 – 1992 alikuwa Mhaidrolojia na baadaye Mhaidrojiolojia Mwandamizi.

Kati ya mwaka 1993 na 1995 alikuwa Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Strengthening the Ministry Towards Achieving the International Drinking Water Supply and Sanitation Decade. Mwaka 1996 hadi 1999 alikuwa Mratibu wa Mradi wa Support to Water Sector Coordination. Mnamo mwaka 2000–2001 alikuwa Mhaidrojilojia Mkuu kwenye Wizara kabla ya kujiunga na Wakala wa Uchimbaji wa Visima na Ujenzi wa Mabwawa kama Meneja wa Ufundi mwaka 2002 hadi 2009 alipoteuliwa kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Utunzaji na Udhibiti wa Rasilimali za Maji.

Bi. Lupimo ana Shahada ya Uzamili ya Biashara (MBA), 2006 pamoja na Shahada ya Sayansi katika Jiolojia (1984) zote kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alipata Stashahada ya Utafiti wa Maji Chini ya Ardhi mwaka 1991 iliyotolewa na International Institute for Geo-Information Science and Earth Observation (ITC), Uholanzi. Alizaliwa mwaka 1959 na kupata Elimu ya Msingi katika Shule za Msingi za Azimio, Musoma na Kazima, Tabora mwaka 1967-1973; Elimu ya Sekondari na Elimu ya Juu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Jangwani mwaka 1974 hadi 1980.