Wasifu

Agnela Nyoni

Mkurugenzi Idara ya Sera na Mipango

Agnela Nyoni

Bi. Agnela Nyoni aliteuliwa na Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne kuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Usalama wa Raia mwezi Februari, 2008. Bi. Nyoni alihamishiwa katika Wizara ya Usalama wa Raia akitokea Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi alikoanzia kazi mwaka 1986, ambapo alipanda ngazi mbalimbali hadi kufikia ngazi ya Mchumi Mkuu.

Baada ya uamuzi wa Serikali wa kuunganisha pamoja Wizara ya Usalama wa Raia na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, aliendelea kuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi hadi mwaka 2013 alipohamishiwa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Bi. Nyoni ana Shahada ya Uzamili katika Uchumi kutoka The Institute of Social Studies-Uholanzi na Shahada ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Alizaliwa mwaka 1960 Wilayani Mbinga na amesoma Elimu ya Msingi katika Shule ya Msingi Mtama, wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma mwaka 1968-1974 na Elimu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Mtwara mwaka 1975-1978. Elimu ya Juu ya Sekondari aliipata katika Shule ya Sekondari ya Ndanda iliyopo wilayani Masasi, mkoani Mtwara mwaka 1979-1981. Aidha, mwaka 1981-1982 alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria katika Kambi ya Ruvu.