Wasifu

Barnabas Ndunguru

Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu

Barnabas Ndunguru

Bw. Barnabas B. Ndunguru Alizaliwa tarehe 30 Oktoba, 1962 mkoani Ruvuma. Ana Shahada ya Uzamili katika masuala ya Utawala kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe; Shahada ya Uhusiano wa Kimataifa na Utawala kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Amehudhuria kozi mbalimbali za masuala ya Utawala na Uongozi. Amehitimu Elimu ya Msingi katika Shule ya Msingi Pamba, mkoani Mwanza (1978); Elimu ya Sekondari katika Shule ya Lake, mkoani Mwanza (1982); Elimu ya Juu ya Sekondari katika Shule ya Umbwe, mkoani Kilimanjaro (1985); na amehudhuria mafunzo ya mwaka mmoja katika Jeshi la Kujenga Taifa Makutupora, Dodoma (Julai, 1985 hadi Jun,i 1986).

Bw. Ndunguru ni mtumishi mwandamizi, mbobezi katika masuala ya Utawala na Maendeleo ya Rasilimali Watu anayeamini katika falsafa ya ‘kutumikia kwanza’.