Utaratibu wa Kuchimba Mabwawa

1.0 Utaratibu kwa Wananchi/Wanakijiji

Utaratibu ufuatao unatakiwa kufuatwa ili kujengwa bwawa kwa ajili ya mwananchi/wanakijiji:

(i) Kuibua mradi

Wananchi/wanakijiji wa sehemu husika wanapaswa kuibua mradi wa bwawa kwa kumuandikia Mkurugenzi wa Halmashauri juu ya uhitaji wa mradi wa bwawa au kuibuliwa kwa mradi kunaweza kutokana na ahadi za viongozi wa juu wa Serikali wakati wa ziara katika eneo husika. Viongozi hao ni kama Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Maji na Naibu Waziri wa Maji.

(ii) Eneo Linalofaa Kujengwa Bwawa, Upimaji na Usanifu

Kama ombi la mradi linakuwa limewasilishwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri na kama Halmashauri ina Mtaalam/Wataalam wa mabwawa inatakiwa, Mkurugenzi wa Halmashauri kutuma Mtaalam/Wataalam katika eneo husika kwa lengo la kutafuta eneo linalofaa kujengwa bwawa ikiwa ni pamoja na kuangalia upatikanaji wa karibu wa material ya kujengea. Mtaalam/Wataalam wanatakiwa kuwasilisha taarifa ya awali (Preliminary/ Recconnainses Survey Report).

Kama Mkurugenzi wa Halmashauri hana wataalam wa mabwawa inabidi kuomba watalam Wizara ya Maji ambao watafanya preliminary/ recconnainses survey kisha kuendelea na usanifu wa kina kama ni bwawa dogo na la ukubwa wa wastani. Kama bwawa ni kubwa timu ya Wataalam wa mabwawa inabidi kuandaa hadidu za rejea kupitia Preliminary/ Recconnainses Survey Report kwa lengo la kufanya manunuzi ya Mtaalam Mshauri atakae fanya kazi ya usanifu wa kina.

(iii) Ujenzi wa Bwawa

Kabla ya ujenzi kuanza, inahitajika kufanyika taratibu za manunuzi wa Mkandarasi wa ujenzi na Mtalaam Mshauri au kuunda kikosi kazi cha Wizara na Halmashauri kwa lengo la kusimamia ujenzi. Baada ya manunuzi, Mkandarasi atasaini mkataba na atakabidhiwa eneo la mradi tayari kuanza ujenzi.

2.0 Utaratibu kwa Mtu Binafsi/Kampuni Binafsi

Utaratibu ufuatao unatakiwa kufuatwa ili kujengwa bwawa kwa ajili ya mtu/kampuni binafsi:

(i) Kuibua mradi

Mtu binafsi/Kampuni binafsi anahitajika kuibua mradi wake kwa kuandaa pendekezo (proposal) na kujaza fomu za kuomba kibali cha ujenzi wa bwawa kisha kuwasilisha Wizara ya Maji Kuomba kibali. Wizara ya Maji kupitia Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji ataagiza Kitengo cha Usalama wa Mabwawa kutembelea eneo husika, kutoa ushauri na kutoa kibali cha kuendelea na hatua zingine za ujenzi kama itaonekana inafaa.

(ii) Upimaji na Usanifu

Kama ombi la Mtu binafsi/Kampuni binafsi la kujenga bwawa limekubaliwa, hatua inayofuata ni Mtu binafsi/Kampuni binafsi kuwasilisha Wizara ya Maji profile ya Mtalam Mshauri/ Mkandarasi atakae sanifu/kujenga bwawa hilo, wasilisho hilo linatakiwa ikiwa na majina ya wataaalam watakaoshiriki kujenga kupima na kusanifu. Wizara itapitia wasifu wa wataalam wa Mkandarasi/Mtalam Mshauri na itatoa kibali cha ujenzi wa bwawa kama itaonekana inafaa.

(iii) Ujenzi wa Bwawa

Mtu binafsi/Kampuni binafsi inahitaji kuingia mkataba na Mkandarasi/Mtalaam Mshauri aliyepewa kibali na Wizara ya Maji kufanya kazi hiyo kama inavyoeleza hapo juu katika kipengele (ii) kisha kuendelea na ujenzi.