Swahili | English        Barua Pepe
 Maswali |  Viunganishi Muhimu | Ramani ya Tovuti | Wasiliana Nasi        
 
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kinaongozwa na Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta.

Kazi za Kitengo:


• Kusimamia utekelezaji wa sera ya Serikali Mtandao na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Wizara.
• Kuhakikisha vifaa vya kompyuta na mtandao wa mawasiliano vinakuwa katika hali nzuri.
• Kusaidia na kutoa huduma za manunuzi ya vifaa vya kompyuta na Mtandao wa Mawasiliano katika Wizara.
• Kuanzisha na kusimamia matumizi ya mawasiliano ya baruapepe, mtandao wa ndani na nje ya Wizara.
• Kuratibu na kusimamia uanzishwaji wa mifumo ya kompyuta na benki za takwimu katika Wizara.
• Kuratibu na kusimamia uendelezaji wa watumishi katika matumizi ya Technolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA).
• Kufanya tafiti zinazohusiana na utumiaji wa teknolojia ya mawasiliano kama chombo cha kuimarisha utendaji, utoaji wa taarifa muhimu na huduma kwa wananchi na wadau wote.
 


 

   

   

  Programu /  Miradi /  Maelezo /  Zabuni
Nafasi za Kazi /  Hotuba /  Picha
Makala /  Takwimu /  Tafiti /  Nafasi za Uwekezaji