| Kitengo cha Manunuzi |  |
Kitengo cha Manunuzi kinaongozwa na Afisa Ugavi Mkuu.
Kitengo kinajukumu la kutoa huduma na utaalamu katika masuala ya manunuzi, uhifadhi na usambazaji wa huduma na bidhaa kwa Wizara.
Kazi zake:
• Kutoa ushauri kwa menejimenti katika masuala ya manunuzi ya vifaa na huduma.
• Kuhakikisha kuwa Wizara inazikubali taratibu na kanuni za manunuzi kutokana na sheria ya umma ya manunuzi Na.21 ya 2004.
• Kuandaa mpango mwaka wa manunuzi wa Wizara.
• Kununua na kusimamia usambazaji, malighafi na utoaji wa huduma ili kusaidia mahitaji ya Wizara.
• Kuhakikisha kuwa uhifadhi mzuri na usambazaji wa vifaa vya ofisi unatekelezwa kwa muda muafaka.
• Kuwa Katibu wa Bodi ya Manunuzi kama Kanuni za umma za manunuzi zinavyosema.
• Kusaidia Idara na vitengo vya Wizara kupata ubora wa vitu kulingana na bei, ubora na ufikishwaji wa huduma na bidhaa zinazohitajik
|