| |
| Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano |  |
Kitengo kinaongozwa na Afisa Habari Mkuu
Kitengo kinatoa huduma ya upatikanaji wa taarifa, mawasiliano ya Wizara kwa umma na vyombo vya habari.
Kazi zake:
• Kuandaa na kutoa machapisho, vipeperushi, makala, majarida n.k. kwa lengo la kuhamasisha umma juu ya Sera, programu, kazi na mabadiliko yanayotokea ndani ya Wizara.
• Kuratibu mazungumzo ya Wizara na vyombo vya habari.
• Kushiriki katika mijadala ya Wizara na umma pamoja na vyombo vya habari.
• Kuhamasisha utekelezaji wa sera na programu za Wizara.
• Kuratibu maandalizi ya taarifa mbalimbali zinazotolewa kwenye makongamano, mikutano, na vyombo vya habari.
• Kuratibu uandaaji na utoaji wa jarida la Wizara.
• Kuratibu uwekaji wa taarifa katika tovuti ya Wizara.
|
|
|
|