Maji Week 2019

Siku ya Maji

Wizara ya Maji imekuwa ikiratibu Wiki ya maji kitaifa kila mwaka hapa nchini kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya maji. Maadhimisho haya yanatokana na Azimio Na. 47/193 la Umoja wa Mataifa (UN) kuwa kila ifikapo Machi, 22 ya kila mwaka nchi wanachama ziadhimishe siku ya maji Duniani kwa pamoja.

Hii ni Katika kutambua umuhimu na thamani ya maji katika maisha ya binadamu na uchumi wa Dunia kwa ujumla

Lengo kuu la maadhimisho ya Wiki ya Maji nchini ni kuungana na Mataifa mengine katika kutathimni utekelezaji, mafanikio, changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi ya maji na kuainisha mikakati ya kuboresha na kuimarisha utoaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira na kusimamia utunzaji wa rasilimali ya maji nchini.

KAULIMBIU

Kaulimbiu ya Wiki ya Maji mwaka huu ni:

Hakuna Atakayeachwa: Kuongeza Kasi ya Upatikanaji wa Huduma yaMajisafi na Usafi wa Mazingira kwa Wote katika dunia inayobadilika kitabia nchi

Maadhimisho ya wiki ya maji mwaka huu yataanza 16-22 Machi, 2019 na tarehe 22 Machi, itakuwa kilele. Maadhimisho ya siku ya maji kitaifa yatafanyika jijini Dodoma.

Yatakayofanyika Wiki ya Maji Kitaifa jijini Dodoma

Siku ya Maji Duniani: Maji ni Kichocheo cha Maendeleo

Book of Abstracts: Maji Week 2019, Annual Scientific Conference