Habari

Imewekwa: Mar, 19 2019

Utunzaji Rasimali za Maji: Wataalam watakiwa kutoa elimu zaidi

News Images

Wataalam katika sekta ya maji wanaohuduhuria Kongamano la Kisayansi Kuhusu Sekta ya Maji nchini wametakiwa kutoa elimu kuhusu utunzaji wa rasilimali za maji ambayo haiongezeki ilhalimahitaji yake yanaongezeka kila siku.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo amesema hayo jijini Dodoma wakati akiongea na Wataalam na washiriki wa kongamano hilo lililofanyika kwa siku mbili ikiwa ni moja ya matukio ya Wiki ya Maji kitaifa kwa mwaka 2019.

Prof. Mkumboamesema miongoni mwa miji inayokua kwa kasi hivi sasa ipo Barani Afrika na kama hatua hazichukuliwa mapema uhaba wa maji utaikumbuka baadhi ya miji ifikapo mwaka 2050. Amesema ni vizuri wataalam wakatumia elimu yao kuwashirikisha wananchi na kutoa elimisha zaidi kuhusu utunzaji wa rasilimali za maji.

Prof. Mkumbo amesema ni vizuri kujenga utamaduni wa kuwa na jukwaa la kuwashirikisha watu wengine kuhusu uzoefu na utaalam pamoja na utafiti katika sekta ya maji ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utendaji kazi, na kuhudumia wananchi vizuri zaidi.

Kufuatia wazo hilo, wataalam na washiriki wa Kongamano la Kisayansi wameazimia kuanzisha chapisho la kitaalam, Jarida la Sekta ya Maji, na kumpitisha Prof. Tolly Mbwete kuwa Mhariri Mkuu mwanzilishi, na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo kuwa mlezi wa jarida hilo.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano

19.03.2019