Wakala wa Ujenzi wa Mabwawa na Uchimbaji Visima

Wakala wa uchimbaji wa Visima na Mabwawa ni wakala wa serikali ulioanzishwa chini ya sheria ya wakala wa serikali no 30 ya mwaka 1997. Inafanya kazi chini ya Wizara ya Maji na ilizinduliwa tarehe 26 - 03- 1999 japo ilianza kufanya kazi mwaka 1997.

Wakala wanao wataalamu wenye ujuzi na uzoefu kama vile wahaidrolojia, wahandisi wa uchimbaji, wapimaji wa ardhi, wahandisi wa ujenzi katika fani zinazoendana na uendelezaji na usimamizi usimamizi wa rasilimali za maji.

Wakala wa uchimbaji visima wamefanikiwa miradi mingi hapa nchini hiyo ni pamoja na miradi inayohusu utafiti, usanifu na ujenzi wa mabwawa pamoja na kujenga mifumo ya kusambaza maji. Wakati wa utekelezaji wa miradi wakala inatoa ushauri wa kiufundi pamoja na ushauri mwingine unaohitajika kufanya mradi uwe endelevu. Huduma zitolewazo na Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa ni kama zifuatazo:

 • Kufanya tathmini za sura ya nchi, upimaji wa udongo na usanifu wa mabwawa;
  • Uchunguzi wa maji chini ya ardhi kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
  • Ukusanyaji wa sampuli za udongo ili kufuatilia;
  • Kufunga mashine za pampu zenye kutumia dizeli, jua au umeme (pampu za mchine na mikono);
  • Ujenzi na ukarabati visima virefu;
  • Ujenzi wa mitandao midogo ya usambazaji maji;
  • Kutoa mafunzo kwa jamii juu ya utunzaji wa visima na mabwawa;
  • Ukodishaji wa mashine, mitambo na utengenezaji wa magari;
  • Kutoa ushauri wa kitaalamu.