SERIKALI KUHAMASISHA SEKTA BINAFSI KUSHIRIKI KATIKA MAENDELEO YA SEKTA YA MAJI

SERIKALI KUHAMASISHA SEKTA BINAFSI KUSHIRIKI KATIKA MAENDELEO YA SEKTA YA MAJI

Mahali

Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Tarehe

2018-07-19 - 2018-07-20

Muda

2:00 asubuhi - 10 jioni

Madhumuni

Kujadili fursa zilizopo na changamoto zinazoikabili sekta binafsi nchini katika kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Sekta ya Maji nchini.

Event Contents

Tunapenda kuujulisha umma kuwa Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Washirika wa Maendeleo wa Sekta ya Maji wameandaa Kongamano maalum litakalowakutanisha Serikali na Sekta Binafsi ambao ni wadau wa Sekta ya Maji nchini.

Kongamano hili litafanyika kuanzia tarehe 19 hadi 20 Julai, 2018 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Mada mbalimbali zitawasilishwa na kujadiliwa na hatimaye kuandaliwa maazimio kwa ajili ya kufikishwa katika ngazi mbalimbali za maamuzi na utekelezaji. Matokeo tarajiwa ya kongamano hili ni pamoja na kuongeza idadi ya makampuni binafsi yanayoshiriki katika maendeleo ya Sekta ya Maji; kuongeza ubora wa kazi; na kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maji nchini; na kuongeza mchango wa Sekta ya Maji kwenye Pato la Taifa na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.

Kwa kujisajili tembelea tovuti: www.maji.go.tz


Washiriki

Wakandarasi, Wazalishaji Viwandani, Wataalam Washauri na Viongozi wa Serikali. Pia, wawakilishi kutoka CTI, TPSF, TCCIA, CRB, ERB, TWCC na ACET.

Ada ya Tukio

Hakuna ada ya ushiriki.

Simu

+255652 827 898/784299207 au +255785 585 569

Barua pepe

pppforum@mowi.go.tz