NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA MAJI YA TAIFA

Imewekwa: Jul 13, 2018


Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji anatangaza nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Maji ya Taifa (National Water Board). Bodi hii ni Bodi ya ushauri ambayo inaundwa kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Na. 11 ya mwaka 2009 Kifungu Na. 20. Muda wa Bodi ni miaka mitatu.

MAJUKUMU YA BODI

Majukumu ya Bodi kama yalivyoainishwa kwenye Sheria ni kumshauri Waziri mwenye dhamana ya maji katika masuala mtambuka yanayohusu usimamizi wa rasilimali za maji, mipango shirikishi ya maji (integrated water resourcesmanagement plans), utatuzi wa migogoro ya maji yenye sura ya kitaifa na kimataifa, usimamizi wa rasilimali za maji tunazoshirikiana na nchinyingine (transboundary water resources management) na masuala ya kuhamisha maji kutoka bonde moja kwenda bonde jingine (Inter-basin water transfer).

SIFA ZA MWOMBAJI

Mwombaji wa nafasi hii anatakiwa kuwa na ujuzi na uzoefu katika masuala ya sekta ya maji au sekta zinazohusiana na sekta hiyo. Aidha, awe na ujuzi mahsusi kwenye masuala ya usimamizi wa rasilimali za maji na asiwe/asitoke kwenye taasisi ambayo ni mtumiaji mkuu wa maji (major water user).

Maombi yatumwe kwa :

Katibu Mkuu,

Wizara ya Maji,

Tawi la NBC, Mazengo,

Barabara ya Kuu,

S.L.P. 456,

40473, DODOMA.

Maombi yaambatishwe na wasifu wa mwombaji (CV) yenye wadhamini watatu na namba zao za simu. Andika “Mwenyekiti Bodi ya Maji ya Taifa” nyuma ya bahasha.

Mwisho wa kupokea maombi ni Jumanne tarehe 23 Oktoba, 2018 saa 09.30 alasiri

Imetolewa na:

Prof. Kitila Mkumbo

KATIBU MKUU

WIZARA YA MAJI

09 Oktoba, 2018