| Idara ya Sera na Mipango |  |
Idara ya Sera na Mipango inaongozwa na Mkurugenzi.
Idara ina sehemu tatu:
Majukumu ya Idara hii ni kuandaa Sera kusimamia utekelezaji wake na kupima matokeo ya utekelezaji wa Sera.
Kazi zake ni:
• Kusimamia maandalizi ya bajeti ya Wizara;
• Kusimamia na kupima utekelezaji wa shughuli za Sekta ya Maji na Umwagiliaji ndani na nje ya Wizara ili kuona kama vigezo vya utekelezaji vilivyowekwa vinafuatwa;
• Kutoa miongozo ya kimaamuzi ya mipango ya baadaye ya Wizara;
• Kuhamasisha na kuwezesha sekta binafsi ili ziweze kuwekeza katika sekta ya maji na umwagiliaji;
• Kukusanya taarifa za sekta za maji na umwagiliaji kwa ajili ya maamuzi ya Wizara;
• Kuhusika na maandalizi ya Hotuba ya Wizara na taarifa ya mwaka ya hali ya uchumi;
• Kutoa utaalamu wa mkakati wa pamoja katika kupanga na kubajeti;
• Kuhakikisha mipango na bajeti za sekta za maji na umwagiliaji zinawekwa katika mipango na bajeti ya taifa.
Sehemu ya Sera:
Kazi zake:
• Kuandaa na kupitia kutekelezaji, kupima na kusimamia utekelezaji wa Sera za Wizara;
• Kuratibu na kupitia sera za Wizara na kuziweka katika hali nzuri na kuhakikisha zinahusiana Sera za Taifa;
• Kushauri uandaaji wa nyaraka za kisera zinazoandaliwa na Wizara zingine;
• Kuandaa (memorandum of understanding) za miradi na programu kwa ajili ya ushirikiano na utafutaji wa fedha kimataifa;
• Kuandaa taarifa za utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na maoni ya Kamati ya Bunge;
• Kuratibu maandalizi ya bajeti ya Wizara na Hotuba ya mwaka ya mpango wa bajeti wa Wizara.
Sehemu ya Mipango
Kazi zake:
• Kuratibu uandaaji wa mpango wa mwaka wa utekelezaji na mpango wa mkakati wa muda mfupi na mrefu;
• Kuhusisha miradi ya programu na mipango ya utekelezaji kwa ajili ya utafutaji wa fedha za utekelezaji wa malengo ya Wizara;
• Kutoa miongozo ya kiufundi na kuwezesha uandaaji wa mikakati na mipango ya Wizara;
• Kuwasiliana na Wizara ya Fedha na ukuzaji wa uchumi na ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa umma kuhusu mipango ya Wizara na
• Kushiriki katika uamasishaji wa kazi zinazofanywa na sekta binafsi.
Sehemu ya Usimamizi na ufuatiliaji
Kazi zake:
• Kusimamia utekelezaji wa mpango wa mwaka na mpango mkakati wa muda mfupi wa Wizara;
• Kuandaa taarifa za utekelezaji za wiki, mwezi, robo mwaka, nusu mwaka na za mwaka mzima za Wizara;
• Kushiriki katika maandalizi ya mipango programu na majukumu ya utekelezaji ya Wizara;
• Kutoa msaada wa kiufundi ndani ya Wizara, hii ni pamoja na usimamizi na ufuatiliaji katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara;
• Kufanya ufuatiliaji wa huduma inayotolewa na Wizara kwa Wadau;
• Kuratibu utekelezaji wa nusu mwaka na wa mwaka mzima wa malengo ya Wizara na
• Kufuatilia utendaji wa wakala za Wizara.
|