Swahili | English        Barua Pepe
 Maswali |  Viunganishi Muhimu | Ramani ya Tovuti | Wasiliana Nasi        
 
Idara ya Maabara za Maji

Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi

Maabara za Maji ni moja kati ya Idara za Wizara ya Maji na Umwagiliaji, inajukumu la kusimamia ubora wa vyanzo vya maji na kuzuia uchafuzi wa vyanzo hivyo. Idara ina vituo16 vya maabara za maji nchini, vituo hivyo ni: Arusha, Bukoba, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kigoma, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Musoma, Singida, Shinyanga, Songea, Sumbawanga na Tanga.

Vilevile inahusika na uchunguzi wa ubora wa kemikali zinazotumika katika kutibu maji, lengo ni kuhakikisha kuwa kemikali hizo zinaviwango vinavyotakiwa.

Kazi zake ni:

• Kuchunguza muonekano, kemikali, vijidudu katika maji kwa matumizi ya viumbe hai;
• Kuchunguza majitaka ili kujua kama yanafaa kuchanganywa katika vyanzo vingine;
• Kuchunguza kemikali zinazotumika katika kutibu maji ili kujua ubora wake na kuishauri jinsi ya kuzitumia;
• Kuchunguza kemikali katika udongo na kushauri wajenzi na shughuli za kilimo kuhusiana na kemikali;
• Kufanya tafiti zinazohusiana na ubora wa maji.

 


 

   

   

  Programu /  Miradi /  Maelezo /  Zabuni
Nafasi za Kazi /  Hotuba /  Picha
Makala /  Takwimu /  Tafiti /  Nafasi za Uwekezaji