Swahili | English        Barua Pepe
 Maswali |  Viunganishi Muhimu | Ramani ya Tovuti | Wasiliana Nasi        
 
Idara ya Umwagiliaji na Huduma ya Ufundi

Idara ya Umwagiliaji na Huduma ya Ufundi inaongozwa na Mkurugenzi.

Jukumu lake ni kutoa utaalamu katika kuendeleza miundombinu ya umwagiliaji na usimamizi bora wa maji ili kuongeza uzalishaji katika kilimo hapo nchini.

Kazi zake ni:

• Kuandaa Sera ya Maendeleo ya Kilimo cha Umwagiliaji, mikakati na kusimamia utekelezaji wake;
• Kuhamasisha maendeleo na ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji nchini;
• Kuzijengea uwezo Serikali za Mitaa ili ziweze kusimamia miradi ya kilimo cha umwagiliaji;
• Kufuatilia na kusimamia ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji;
• Kutoa msaada wa kifedha na kiufundi katika ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya umwagiliaji;
• Kuchochea na kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi katika kuendeleza kilimo cha umwagiliaji;
• Kuhakiki na kudhibiti ubora wa kiufundi katika maendeleo ya miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji.

Sehemu ya Mipango na Usanifu
Kazi zake ni:
• Kuainisha maeneo yanayofaa kilimo cha umwagiliaji;
• Kuhamasisha huduma na miradi ya umwagiliaji;
• Kusanifu na kuandaa mipango ya miradi ya umwagiliaji;
• Kuandaa kabrasha za zabuni za manunuzi;
• Kuandaa miongozo ya kiutendaji na matengenezo;
• Kusaidia katika uanzishwaji wa vikundi vya umwagiliaji;
• Kuandaa sera na mikakati ya maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji;
• Kutoa ushauri katika kusanifu na mipango ya kilimo cha umwagiliaji;
• Kusanifu na kuandaa mipango ya matumizi ya maji chini ya ardhi na juu ya ardhi kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.

Sehemu ya Usimamizi wa Ujenzi na Miundombinu
Kazi zake ni:
• Kudhibiti na kusimamia ubora wa miundombinu ya umwagiliaji;
• Kusimamia ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya miradi ya umwagiliaji;
• Kufuata viwango vya ujenzi na kufikisha sifa za viwango hivyo kwa wajenzi wa miradi ya umwagiliaji;
• Kuandaa na kusambaza miongozo ya utendaji na matengenezo;
• Kusimamia mikataba ya miradi ya umwagiliaji;
• Kuhakikisha tathmini ya mazingira inafanyika wakati wa ujenzi wa miradi;
• Kutoa msaada wa kiufundi katika taasisi binafsi kuhusu ujenzi wa miradi ya umwagiliaji;
• Kuhamasisha tafiti mpya/njia mpya za miradi ya umwagiliaji;
• Kuhifadhi benki ya takwimu ya miradi ya umwaguliaji;
• Kuzijengea uwezo Halmashauri za Wilaya katika utekelezaji wa miradi ya umwagiliaji.

Sehemu ya Utafiti na uendeshaji wa kilimo cha Umwagiliaji
Kazi zake ni:
• Kuhamasisha matumizi ya tafiti zilizokubalika za kilimo cha umwagiliaji;
• Kuhamasisha matumizi ya teknolojia zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji;
• Kuhakikisha teknolojia zinazofaa, zenye bei nafuu na zinazotumia maji vizuri, zinatumika katika kilimo cha umwagiliaji;
• Kuhamashisha matumizi ya nishati mbadala kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji;
• Kuhamasisha matumizi ya njia za kienyeji ambazo zinakubalika katika kilimo cha umwagiliaji ili kupunguza gharama za uzalishaji na upotevu wa maji;
• Kushirikiana na taasisi zinazofanya tafiti katika kuendeleza tafiti mbalimbali za kilimo cha umwagiliaji;
• Kufikisha tafiti mpya za maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji kwa wananchi na
• Kushirikiana na sekta binafsi na watoa huduma wengine katika kuhakikisha kuwa maji yanatumika vizuri katika kilimo cha umwagiliaji.


 


 

   

   

  Programu /  Miradi /  Maelezo /  Zabuni
Nafasi za Kazi /  Hotuba /  Picha
Makala /  Takwimu /  Tafiti /  Nafasi za Uwekezaji