Swahili | English        Barua Pepe
 Maswali |  Viunganishi Muhimu | Ramani ya Tovuti | Wasiliana Nasi        
 
Idara ya Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu

Idara ya Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu inaongozwa na Mkurugenzi.

Kazi zake ni:
• Kutoa mikakati ya kimenejimenti katika utawala na maendeleo ya rasilimali watu kama vile kuajiri, mafunzo, kuhamasisha kutoa huduma kwa watumishi na usimamizi wa katika utendaji;
• Kuhakiki usimamizi wa rasilimali watu katika Wizara;
• Kuunganisha kati ya Wizara na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma katika utendaji wa menejimenti ya utumishi wa umma;
• Kutoa huduma ya maelezo na kutunza kumbukumbu za taarifa za rasilimali watu.

Sehemu ya Usimamizi ni:

• Kutafsiri kanuni za huduma za umma, kanuni “Standing Order” na sheria zingine za kazi;
• Kusimamia uhusiano mzuri wa wafanyakazi na ustawi pamoja na afya, usalama, michezo na utamaduni;
• Kutoa usajili, kuweka kumbukumbu za Ofisi na huduma za wahudumu;
• Inasimamia masuala ya kanuni.
• Kutoa huduma za ulinzi, usafiri na mambo mengine ya kiutawala kwa ujumla;
• Kutekeleza mambo mbalimbali ikiwemo jinsia, wasiojiweza, Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi na Ukimwi;
• Kufuatilia utekelezaji wa ushiriki sekta binafsi katika Wizara;
• Kusimamia jukumu la utekelezaji wa mkataba wa huduma kwa wateja wa Wizara.

Sehemu ya menejimenti ya Rasilimali Watu

• Inasimamia zoezi zima la ajira ikiwemo kukusanya, kuchagua, kuchukua, kuthibitisha kazini pamoja na uhamisho;
• Inahusika na maendeleo na mafunzo ya rasilimali watu;
• Inasimamia mafunzo ya awali na programu za utangulizi kwa waajiriwa wapya;
• Kuweka mipango ya rasilimali watu ili kujua mahitaji na idadi ya wataalamu walio chini ya Wizara;
• Kusimamia mishahara na kuandaa idadi ya watu wote walioajiriwa;
• Kusimamia utekelezaji wa malengo na mfumo wa wazi wa kupima utekelezaji wa watumishi wa Wizara.
 


 

   

   

  Programu /  Miradi /  Maelezo /  Zabuni
Nafasi za Kazi /  Hotuba /  Picha
Makala /  Takwimu /  Tafiti /  Nafasi za Uwekezaji