Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maji na Umwagiliaji yapata Uongozi Mpya

Swahili

Wizara ya Maji na Umwagiliaji imepata uongozi mpya mara baada ya mabadiliko madogo yaliyofanywa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli  kwenye Baraza lake la Mawaziri.

Rais Magufuli amemteua Inj. Isack Kamwelwe aliyekuwa Naibu Waziri katika Wizara hiyo, kuwa Waziri mpya na Jumaa Aweso kuwa Naibu Waziri.

 Viongozi hao wamewasili katika ofisi ndogo za Wizara zilizopo Ubungo Maji, jijini Dar es Salaam mara baada ya kula kiapo na kupokelewa na uongozi wa wizara ukiongozwa na Katibu Mkuu, Prof. Kitila Mkumbo.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Kamwelwe aliishukuru Wizara kwa kumpa ushirikiano mzuri akiwa Naibu Waziri na kuahidi ushirikiano wa karibu kutoka kwake kama Waziri.

Kadhalika, Naibu Waziri, Jumaa Aweso alishukuru kwa mapokezi mazuri na kuomba ushirikiano wa Wizara, ili kwa pamoja waweze kuleta maendeleo kwenye Sekta za Maji na Umwagiliaji.

Photo: