Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taarifa kwa vyombo vya Habari

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Malawi zimekubaliana kuanzisha Kamisheni ya Kuendeleza Bonde la Mto Songwe. Makubaliano hayo yalitiwa saini kati ya Mawaziri wanaohusika na Maji na Umwagiliaji katika mkutano wa wawekezaji wa kuendeleza bonde hilo uliofanyika wiki iliyopita jijini Lilongwe, nchini Malawi katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Bingu. 

Kongamano hili lililenga kuwashawishi wawekezaji na washirika wa maendeleo kuwekeza na kufadhili miradi itakayotekelezwa kwa kipindi cha miaka 10 ya Awamu ya Tatu ya Programu ya Kuendeleza Bonde la Mto Songwe kuanzia mwaka 2017 inayokadiriwa kugharimu Dola za Marekani milioni 829.  

Makubaliano ya kuanzisha kamisheni yalitiwa saini na Mawaziri wanaohusika na masuala ya Maji na Umwagiliaji wa nchi hizi. Mawaziri hao ni Mhe. Mhandisi Gerson H. Lwenge (MB) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mhe. Aggrey C. Masi (MB) wa Jamhuri ya Malawi. Tukio hili la kusaini lilishuhudiwa na Prof. Kitila Mkumbo, Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Tanzania, Mhe. Balozi Victoria Mwakasege, Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Bi. Erica Maganga, Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji na Maendeleo ya Maji, Malawi, pamoja na wadau waliohudhuria kongamano hilo.

Miradi inayotarajiwa kutekelezwa katika bonde hili ni pamoja na ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme (megawati 180.2), kilimo cha umwagiliaji, (hekta 6,200) usambazaji wa maji kwa wananchi, ujenzi wa miundombinu ya jamii (bararabara, shule, na vituo vya afya). Miradi mingine ni uanzishaji wa viwanda vidogo na vya kati, uvuvi, utalii na uboreshaji wa mazingira, hususan kuimarisha kingo za mto ambao ni mpaka wa nchi zetu mbili.

Baraza la Mawaziri wa Maji Afrika (AMCOW) linalofanya kazi pamoja na Tume ya Umoja wa Afrika chini ya Idara ya Uchumi Vijijini na Kilimo (AUC-DREA) na Nchi Wanachama wanafanya harakati za kuhakikisha lengo la Usalama wa Maji na Usafi wa Mazingira linafikiwa ulimwenguni. Azma hii imelenga kuhakikisha kunakuwa na misingi imara ya usimamizi, utunzaji na uendelezaji wa rasilimali za maji kwa ajili ya wote, pamoja na hatua sahihi za usafi wa mazingira na afya ya mwanadamu. 

Sekretarieti ya AMCOW kwa kushirikiana na Wizara ya Maji na Umwagiliaji itaandaa Maadhimisho ya 6 wa Wiki ya Maji ya Afrika na Mkutano Mkuu wa 10 wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Afrika, jijini Dar es Salaam, Tanzania chini ya kaulimbiu isemayo 'Kufikia Lengo la Maendeleo Endelevu (SDGs) juu ya Usalama wa Maji na Usafi wa Mazingira'.

Kwa maelezo zaidi bonyeza hapa

Wizara ya Maji ikishirikiana na OWM -TAMISEMI, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya mbalimbali zimepata mafanikio makubwa katika utekelezaji wa mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa kwa kuwapatia maji wananchi waishio vijijini wapatao 752,000 wa ziada katika kipindi cha miezi mitatu tangu tarehe 1 Julai mwaka huu.
Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 2 ya wakazi wote wanaoishi vijijini kupata huduma ya maji safi kwa kipindi hicho cha miezi mitatu. Baadhi ya miradi iliyokamilika ni ya vijiji vya Mtandi, Rondo, na KinengÔÇÖene vilivyopo Mkoani Lindi; Vijiji vya Engagile, Gedamar, Mtuka vilivyopo Mkoani Manyara; na Vijiji vya Iwalanje, na Maninga vilivyopo Mkoani Mbeya. Hivi ni baadhi tu ya vijiji ambavyo miradi imekamilika na wanavijiji wanapata huduma ya majisafi na salama karibu na makazi yao.

Kwa maelezo zaidi bonyeza hapa 

Kwa wiki kadhaa sasa, kumejitokeza wimbi la vitendo vya kitapeli la kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) pamoja na kupiga simu kwa baadhi ya Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Majitaka Mijini katika Mikoa mbalimbali wakijitambulisha wao ni Mhe Waziri wa Maji au Mhe. Naibu Waziri wa Maji na kuwa wanahitaji msaada wa fedha au wao wametumwa na vingozi hao.