Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji akagua Vyanzo na Mradi wa Maji Njombe

Swahili

Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji Mh. Isack Kamwelwe alifanya Ziara ya kukagua maendeleo ya mradi mpya wa Kibena, eneo la kujenga mradi mpya wa Hagafilo na vyanzo vikuu viwili vya chemchem za Nyenga na Magoda vinavyohudumia Maji kwa wakazi wa Njombe Mjini.

Katika ziara hiyo Mhe  Kamwelwe alitembelea kazi mbali mbali za mradi, ujenzi wa matenki na ulazaji wa bomba pamoja ofisi ya NJUWASA na Halmashauri ya Mji.

Mradi wa Kibena unajengwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia NT business network Tanzania limited unaohusisha ulazaji wa mabomba ya ukubwa mbalimbali kwa kilomita 2.1 kutoka kwenye chanzo mpaka tenki lilipo na ujenzi wa tegeo la Maji pamoja na upanuzi wa Nyumba ya kuhifadhi pampu. 

Lengo ni kuongeza uzalishaji kufikia mita za ujazo 1728 kwa siku kutoka 384 kwa siku. Kazi hii itakapokamilika inatarajiwa itagawa Maji kwa wakazi wa Kibena, hospitali teule ya Kibena na maeneo mapya kama Mpeto.

Hadi utakapokamilika mradi utaghalimu Tsh.1,108,301,421  kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji. Mradi huo unatarajiwa kukamilika Novemba 30 2017.

Baada ya kukamilisha kujenga mradi wa kuboresha huduma ya Maji Kibena, awamu ya kwanza kutakuwa na mradi wa kuboresha huduma ya Maji Kibena awamu ya pili itakayohusisha

(a)Ulazaji wa mabomba ya usambazaji Maji yenye umbali upatao kilomita 22.5

(b) Ujenzi wa tenki la kuhifadhia Maji lenye ujazo wa lita 135000 Ili tuweze kuwafikia walengwa. ambapo mradi huu utagharimu  Tsh. 1,300,000,000

Aidha Mh.kamwelwe alitembelea chanzo cha mto Hagafilo ambapo tunatarajia kujenga mradi mwingine mkubwa utakaoleta suluhisho la kudumu la tatizo la Maji Mjini Njombe.

Maji hayo yanatarajiwa kugawa Maji mji mzima wa Njombe ukijumuisha maeneo mapya.

Mradi wa Maji kutoka Mto Hagafilo ,chini ya programu ya maendeleo ya sekta ya Maji (WSDP), Mradi huu unatarajiwa kujengwa mara baada ya kupata fedha kutoka serikalini kupitia serikali ya India. Mradi huu utaghalimu kiasi cha USD 36,092,982.23 sawa na karibu shilingi bilioni 80,877,301,782.51 za kitanzania.

Mh.Naibu Waziri alituhakikishia kuwa fedha za kujengea  huo zitapatikana kwa sababu chanzo cha Mradi huo ni cha uhakika na kudumu.

Mh. Naibu waziri alihitimisha kwa kuwapongeza wananchi wa Njombe na kuwasisitiza zaidi juu ya kutunza Mazingira na kuwapongeza NJUWASA kwa kuvisimamia vyanzo vya Maji vizuri na hatua iliyofikia ya mradi huo 80% inaoendana na kasi ya serikali ya sas

Photo: