Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Naibu Waziri Aweso akagua Miundombinu ya Maji Ubungo

Swahili

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji amefanya ukaguzi wa miundombinu ya maji eneo la Ubungo na kujionea miundombinu hiyo ambayo mingi imepasuka na kuvujisha maji mengi kutokana na uchakavu au kuhujumiwa miundombinu hiyo. Katika maeneo aliyopita ameweza kuona upotevu mkubwa wa maji unaotokana na mabomba yaliyopasuka kuvuja, na kusababisha maji mengi kupotea baada ya kuwafikia wananchi kwa ajili ya matumizi.

Naibu Waziri Aweso alisema ipo haja ya kuchukua hatua na kuhakikisha miundombinu hiyo inafanyiwa ukarabati, ili kudhibiti tatizo la upotevu wa maji ambalo limekuwa changamoto kubwa jijini Dar es Salaam.

“Nitakaa na taasisi za DAWASA na DAWASCO tuweke mikakati ya kutatua changamoto hii, ili kuhakikisha kiwango cha upotevu wa maji kinapungua, kwa kuwa ni moja sababu ya wananchi kukosa maji ya uhakika, kwa kuwa mengi yanapotea baadala ya kuwafikia walengwa”, alisema Naibu Waziri.

Photo: