Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mhandisi wa Maji Asimamishwa Kazi

Swahili

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwele amemwagiza Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji kumsimamisha kazi mara moja Mhandisi Goyagoya Mbena aliyehusika katika tuhumu za kusaini barua kwa niaba ya katibu Mkuu ambayo ilitumika kumpata mkandarasi wa kutekeleza mradi wa maji wenye thamani ya Tsh. Bilion 7.4 katika kijiji cha Kamwanda kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.

“Kutokana na uzito wa jambo hilo, kwa mamlaka niliyopewa kisheria kama Waziri wa Maji na Umwagiliaji, ninamwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagilaji kumsimamisha kazi mara moja Mhandisi Goyagoya Mbena aliyehusika katika tuhuma hizi ili kupisha uchunguzi na nipate taarifa ya utekelezaji wa maagizo haya ndani ya siku nne kuanzia tarehe ya taarifa hii” alisema Waziri Kamwele.

Aidha Waziri alitoa wito kwa watumishi wote wa Wizara kuzingatia taratibu kanuni na sheria zilizopo katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku

Photo: