Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Hatutasita Kumchumkulia Hatua Mkandarasi Yeyote Atakayekwamisha Utekelezaji wa Miradi ya Maji

Swahili

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amesema Wizara yake haitasita kumchukulia hatua mkandarasi yeyote endapo atabainika kuwa chanzo cha kukwamisha utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo mbalimbali nchini. Aweso alizungumza hayo wakati akiwa ziarani katika mkoa wa Songwe, akikagua miradi ya maji katika Wilaya ya Momba.  Akiwa kwenye mradi wa Sogea uliopo katika mji mdogo wa Tunduma, amesema endapo mkandarasi wa Kampuni ya Best One aliyepewa kazi ya kujenga mradi huo atashindwa kukamilisha kwa wakati, hawatasita kumchukulia hatua mara moja. ‘‘Serikali inataka mradi huu wa Sogea na miradi mingine yote ya maji nchini ikamilike kwa wakati na wananchi waanze kufaidi matunda ya Serikali yao, ndio maana nipo hapa kufuatilia hilo na wakandarasi waliopewa kazi wahakikishe wanafanya kazi usiku na mchana ili kufanikisha hilo,’’ alisema Naibu Waziri Aweso.

Wakati huo Aweso ameagiza ameagiza Sh. bilioni 1 zilizotolewa na Rais John Magufuli kwa ajili ya ujenzi mradi wa maji Sogea zitumike kwa uadilifu na kukamilisha mradi huo ili kumaliza kero ya maji kwa wakazi wa Sogea na maeneo ya jirani. Naye Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Iranda ameiagiza Idara ya Maji wilayani humo, kutowapa tenda wakandarasi waasio na sifa ambao wanatuhumiwa kukwamisha juhudi za Serikali katika kukabiliana na tatizo la maji, na atakayefanya hivyo atakuwa amevunja sheria na atachukuliwa hatua. Hii inatokana na taarifa kuwa baadhi ya miradi ya maji wilayani Momba kushindwa kukamilika kwa wakati kutokana na uwezo mdogo wa kitaalamu kwa baadhi ya wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo.

Photo: