Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Aweso Awapa Matumaini Wakazi wa Mlimba

Swahili

Jumaa Aweso amewapa matumaini ya kumaliza kero ya maji wakazi wa kata ya Mlimba, iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro alipofika kujionea kilio cha wananchi hao kwa muda mrefu kuhusiana na maji.  Aweso amejionea changamoto kubwa ya maji Mlimba na kuagiza kuchimbwa visima viwili virefu vya maji, ambavyo vitapunguza kero hiyo kwa wakazi wapatao 18,000 kama suluhisho la haraka, huku wakisubiri mradi mkubwa wa mserereko. Aweso amekuwa Naibu Waziri wa kwanza wa Maji kufika katika Kata ya Mlimba na kukagua miradi ya maji na umwagiliaji inayotekelezwa na Serikali.

Photo: