Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Aweso Akagua Maendeleo ya Utekelezaji wa Mradi wa Maji Longido

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ametembelea mradi wa maji wa Longido, katika Jiji la Arusha kwa lengo la kuangalia maendeleo ya utekelezaji wake.

Naibu Waziri Aweso ameweza kujionea maendeleo ya mradi huo kwa kukagua ujenzi wa chanzo cha maji cha Mto Simba, kilichopo wilayani Siha, katika mkoa wa Kilimanjaro, ulazaji wa mabomba yenye umbali wa kilomita 65 mpaka Longido na ujenzi wa tenki la maji la lita 450,000.

Mradi wa maji wa Longido unatekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kusimamiwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA), ni miongoni mwa miradi mikubwa inayotekelezwa na fedha za ndani za Serikali unaotarajiwa kugharimu kiasi cha Sh. bilioni 15.8 na kukamilika Mei, 2018.